News

Jaji Kaijage Apongeza Maandalizi Wilaya ya Hai

Jaji Kaijage Apongeza Maandalizi Wilaya ya Hai

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistoclas Kaijage amepongeza hatua iliyofikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Hai kwenye maandalizi ya mchakato wa Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Jaji Kaijage ametoa pongezi hizo alipotembelea kituo cha mafunzo ya Wataalamu watakaohusika na zoezi la Kuboresha daftari hilo yanayofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa la KKKT Hai Mjini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambaye ndiye Afisa Uandikishaji wa Wilaya amemwakikishia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa wilaya yake imejiandaa vizuri na wataalamu wapo tayari kutekeleza jukumu la muhimu walilokabidhiwa.

Kwa upande mwingine washiriki wa mafunzo hayo ambao ndio watakaotekeleza jukumu la Kuboresha daftari wameishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwaamini na kuwateua kutekeleza kazi hiyo na kuahidi kuitekeleza kwa moyo wa kizalendo kwa manufaa ya nchi na watu wake.

Zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linatarajiwa kufanyika nchi nzima likianzia mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Demo

Related Articles

Leave a Reply

Close