News

DC Hai Arudisha Mashamba ya Wakulima Yaliyoporwa

DC Hai Arudisha Mashamba ya Wakulima Yaliyoporwa

SERIKALI wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imemnyanga mwekezaji Cuthberth Swai mashamba anayodaiwa kuyapora kwa wananchi wa kijiji cha Kimashuku kwa madai kuwa alipewa na serikali ya kijiji hicho kwa ajili ya kulinda mazingira.

Mkuu wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa bibi Mary Manjau aliyefika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya na kulalamikia mwekezaji huyo anayedaiwa kuvamia eneo hilo na kujenga mabanda ya kufugia mbwa na kuweka mawe.

Pamoja na bibi huyo wapo wanachi wengine zaidi zaidi ya 19 ambao wamebainika leo baada ya Mkuu wa wilaya kutembelea eneo hilo na hivyo kumfanya mkuu wa Wilaya kuagiza wananchi wote waliovamiwa kwenye eneo lao na mwekezaji huyo warudishiwe maeneo yao.

“Nilipokea malalamiko kutoka kwa bibi huyu (Mery Manjau) wiki tatu zilizopita na alikuwa akilalamikia eneo lake akidai limeingiliwa na kuvamiwa na Cathbert Swai, kama alivyoeleza hapa alikuwa amelima maharage ya msimu lakini Cathbert akaja na kujenga banda la mbwa kwa maelezo kuwa amepewa eneo hili na serikali ya kijiji ili atunze mazingira na akija ofisi ya kijiji anasema eneo hili amepewa na Mkuu wa mkoa tangu mwaka 1995.” amesema Sabaya.

Ole Sabaya amesema kuwa, Swai alivamia mashamba hayo yenye ukubwa wa zaidi ya hekari 15 na kufanya shughuli za utalii ikiwemo kufuga wanyama kinyume na taratibu za nchi huku eneo la bibi Mary likiwa ni zaidi ya ekari moja.

Mkuu wa wilaya amesema baada ya kupokea malalamiko hayo aliunda kamati kufanyia kazi malalamiko hayo kamati ambayo iliwajumuisha wataalamu mbalimbali akiwemo Mwanasheria, Afisa ardhi na mwenyekiti wa kamati hiyo akiwa ni Katibu tawala wilaya na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamati hiyo iliyoonesha kuwa eneo hilo kihistoria linamilikiwa na bibi Mary na kupendekeza Mwekezaji huyo kuondoa kibanda cha nyavu na mawe yaliyopo kwenye eneo hilo, alipe fidia ya mazao yaliyoharibiwa na ngamia aliowaachia na kula mazao yaliyokuwa shambani na akabidhi maeneo yote anayodai kupewa na serikali ya kijiji

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ameeleza kushangazwa na kitendo cha mwekezaji huyo kuanza kusambaza video kwenye mitandao ya kijamii kuhusu tuhuma za kupokea fedha kiasi cha shilingi milioni 10 ikiwa ni baada ya mwekezaji huyo kupokea taarifa za utekelezaji wa maagizo hayo na kuhoji alikuwa wapi tangu mwaka jana mwezi wa nane asitoe taarifa kwa mamlaka husika.

Naye bibi Mary Manjau amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa hatua hiyo ambayo amesema inasaidia wanyonge waliokuwa wakionewa na watu wenye fedha

Diwani wa kata ya Mnadani Nasib Mndeme amesema kuwa mashamba hayo wananchi waligawiwa na serikali tangu mwaka 1971.

Demo

Related Articles

Leave a Reply

Close