News

Bashiru Ataadharisha Kuhusu Utitiri wa Habari

Bashiru Ataadharisha Kuhusu Utitiri wa Habari

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM taifa Dkt Bashiru Ally amewataka wananchi kupokea taarifa kutoka kwenye vyanzo rasmi ili kuepuka kuvuruga nchi kwani kwa sasa kuna utitiri wa taarifa.

Dkt Bashiru ameyasema hayo leo katika mkutano wa ndani wa chama hicho uliofanyika kwenye  uwanja wa CCM Bomangombe na kutoa wito kwa kila mwananchi kuacha kuziamini taarifa zinazotoka kwenye vyanzo visivyo sahihi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.

Pia Dkt Bashiru amewakumbusha wanasia kufanya siasa safi ikiwa ni pamoja na kujihadhari na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi huku akiwataka wananchi kujitokeza kaika uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

 

Katika upande mwingine katibu wa CCM wilaya ya Hai ndg, Kumotola Kumotola ametumia mkutano huo kumkabidhi Dkt Bashiru wanachama wasiopungua 80 ambao wamekihama chama cha demokrasia na maendeleo chadema na kuhamia CCM.

Dkt Bashiru Ally anafanya ziara ya siku nne mkoani Kilimanjaro na atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa maana ya utekelezaji wa ilani na kuimarisha demokrasia katika chama cha mapinduzi

Demo

Related Articles

Leave a Reply

Close